![]() |
Gazeti la Charlie Hebdo likiwa na katuni ya Mtume Muhammad. |
Gazeti la Kenya limeomba msamaha kwa kuchapisha jalada la gazeti la Charlie Hebdo, kwa kumchora Mtume Muhammad kufuatia kilio kutoka kwa wasomaji Waislamu.
Gazeti la Star “limejutia sana” kwa kosa lolote lililosababishwa na “uchapishaji mpya mdogo” wa jalada.
![]() |
Mchora katuni wa gazeti la Charlie Hebdo Renald Luzier a.k.a Luz akionekana kuguswa na suala hilo wakati wa mkutano na waandishi wa habari. |
Nchini Senegal, serikali imekataza usambazaji wa jarida hilo la Ufaransa.
Wasenegali wengi ambao ni Waislamu wanaonekana kukubali katazo hilo, anasema mwandishi wa habari.
Nchini Ufaransa baadhi wa wasomaji waliamua kurudisha nakala za gazeti hilo.
0 comments:
Post a Comment