Thierry Henry Amtabiria Sanchez Makuu

mpaka sasa Sanchez amefunga magoli 12 kati ya michezo 20 ya ligi kuu nchini Uingereza msimu wa huu wa 2014/15
Straika mkongwe wa klabu ya The Gunners, Thierry Henry 37, ameusifia usajili wa Alexis Sanchez kutoka katika klabu ya Barcelona ya nchini Hispania
na kudai kuwa kwa mtazamo wake ndio usajili bora kabisa kuwahi kufanywa na Mzee Wenger katika kipindi cha miaka sita iliyopita.

Akiongea katika mkutano wa waandishi wa habari katika sherehe za utoaji wa Tuzo za Ballon d’OR alisema;
‘Tangu nilipo ondoka Arsenal mwaka 2007 na kuelekea Barca,
Arsene Wenger amekuwa akijaribu kutafuta aina ya mastraika wenye uwezo wa kuziba pengo langu katika kikosi chake cha kwanza bila mafanikio,
lakini baada ya usajili wa nyota huyu kutoka Chile nadhani ndio suluhisho pekee la makosa ya kiubunifu yaliyokuwa yakifanywa katika eneo la ushambuliaji,
Sanchez anakipaji cha ajabu wa kulijua lango la wapinzani wetu,haitaji kupoteza nafasi nyingi za kufunga iliafunge goli moja,
ninaimani kadiri muda unavyozidi kwenda ndivyo kiwango chake kitavyo zidi kuwa juu,
ukizingatia bado ni mgeni katika ligi hii lakini anaonekana kama tayari ameshakuwa mzoefu wa ligi ya EPL,
nina amini atatoa mchango mkubwa katika kushindania na kushinda vikombe mbalimbali katika pindi chote atakachokipiga akiwa na The Gunners.’
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment